Kusimamia Mali za Bwana Hata Ajapo

Januari | Februari | Machi 2023

Somo La 12

Machi 18 - Machi 24

Thawabu za Uaminifu

  1. Thawabu:

    • Thawabu Yake.

      • Ni akina nani watapokea thawabu zao kutoka kwa Yesu atakapokuja?

        1. watakatifu (Za. 58:11)

        2. Waliopanda haki (Mit. 11:18)

        3. Waliouawa kwa sababu ya imani zao (Mt. 5:12)

        4. Wale wanaowapenda maadui zao (Lk. 6:35)

        5. Wale wenye ujasiri (Eb. 10:35)

        6. Wale wanaomtafuta (Eb. 11:6)

        7. Manabii, watakatifu, walichao Jina Lake (Uf. 11:18)

      • Thawabu itakuwa sawa na matendo ya kila mtu (1Kor. 3:8). Je, hiyo inamanisha tunaokolewa kwa matendo yetu? Hapana kabisa!

      • Wokovu ni karama ambayo kila mmoja anaweza kuipata bila kujali matendo yake (Tit. 3:5). Woye waliokombolewa watapokea “taji” zao, thawabu ya haki (2Tim. 4:8).

    • Uzima wa milele.

      • Ni nini hasa tunachostahili? “Ujira” wetu ni nini? Kifo tu. Ni nini Mungu anachotupatia kama “karama”? Uzima wa milele (Rum. 6:23).

      • Hii ni thawabu tusiyostahili, hatima tofauti kabisa na ile tuliyostaili. Kila mmoja anaweza kuipokea kama ataipokea kwa imani (Yn. 3:16).

    • Kuwa na Yesu.

      • Tuna tumaini kama hilo: kuishi katika Yerusalemu Mpya, mji kwa ajili ya “mataifa ya wale waliokombolewa” (Uf. 21:24). Tutapata nini hapo?

        1. Mkono wa Mungu wa upendo utatufuta machozi yetu. Maumivu na kifo havitakuwepo tena (Uf. 21:4)

        2. Bustani ya Edeni, ambapo tutafika na kula kwenye mti wa uzima (Mwz. 3:22; Uf. 22:2)

        3. Yesu. Tutamwona uso kwa uso (Uf. 22:4)

  2. Uaminifu:

    • Kusimamia kwa ajili ya Bwana…

      • Mfano wa talanta unashughulika na namna tunavyosimamia kile Mungu alichotupatia, katika muktadha wa Wakati wa Mwisho (Mt. 25:14-30).

      • Inatupasa kusimamia talanta zetu za asili, karama ambazo Roho Mtakatifu ametupatia, na kila kitu ambacho Mungu ametupatia. Anatupatia kwa kadri tunavyosimamia.

      • Kila mmoja anawajibika kwa karama na raslimali walizopewa, haijalishi ni ngapi. Thawabu ni ya thamani (Mt. 25:23).

    • hadi Ajapo.

      • Inavyoonekana, Paulo hakuishi maisha ya mafanikio (1 Wakorintho 11:23-28). Na hatujaahidiwa maisha mazuri (2 Tim 3:12)

      • Hata hivyo, Biblia inasemaje kuhusu kuishi maisha ya furaha na mafanikio (1Tim. 6:6-12)?

        1. Siyo kuwa na mali nyingi

        2. Ni kupata kitu wakati unakihitaji

        3. Ni kung’ang’ania ahadi za Mungu

        4. Ni kumshukuru na kumtumainia Mungu

      • Pale Yesu atakaporudi, tutapokea thawabu yetu kwa kusimamia kilicho Chake (2Tim. 4:6-8).

Resource Credit: fustero.es

Zimetafsiriwa na: Daniel Chimagu & Mpoki M. Ulisubisya & Dionize Justine